Huku kwa hamaki nilibamiza mlango wangu
maana nilishajua mama anaweza kuwa
amekasilika kutokana na kitendo cha kuniita muda mrefu. Kutoka tu macho yangu
yaligongana na ujio wa mjomba hapo nilifahamu kuiita kote kule kwa mama ni juu
ya ujio wa mjomba.
"Muda wote mwanangu Criss ulikuwa
unafanya nini cha ajabu huko chumbani?”, punde tu niliponiona mama alianza kwa
kuniuliza swali, kabla hata sijajibu aliendelea kuzungumza. “Haya nenda uchukue
chupa ukamletee mjomba wako soda. Nilifanya kama mama alivyoniambia huku tayari
mjomba alishaipokea salamu yangu ambayo nilitoa kwa sauti ya chini wakati mama
akiendelea kuongea. Kwa muonekano wa
mjomba nilihisi ujio ule haukuwa wa kawaida maana si kawaida yake kuja
nyumbani katika siku kama. Mara nyingi huwa ujio wake unakuwa na jambo
muhimu. Kutoka na mama yangu huwa
mtembeleaji mkubwa wa ndugu zake, na si wengine. Hivyo ujio ule ulinifanya
nitake kujua ni jambo gani haswa lilomleta mjomba nyumbani, roho ya kiudadisi
ilikuwa bado ikinitawala.
Nilingia ndani nikachukua chupa ya soda na kuelekea dukani kwa Mangi. Wakati huo nilimuacha mama akiwa anazungumza na mjomba, mazungumzo ambayo nilikuwa nikitaka kuyafahamu kwa udi na uvumba. Maana ugeni ule ulishanijengea fikra ndani ya kichwa changu, fikra ambazo hazikuwa na majibu sahihi kwangu.
Miguu yangu haikuwa nyuma baada ya
kutoka ndani nilipiga hatua ambazo hazikuwa nyingi hatimaye ni nilikuwa
nimelifikia duka la Mangi na kwa bahati nzuri hakukuwa na foleni kama siku
nyingine. Niliagiza mara moja na kurudi
nyumbani kwa sababu hakukuwa mbali hata si kuchelewa kufika nikampatia ile soda
mjomba. Taratibu mjomba aliendelea kuinywa huku akiendelea kuzungumza na mama.
Nilijivuta pembeni kidogo, na
walipokuwa wakizungumza na kuketi, na kuyatega masikio yangu, masikio nayo
hayakuniangusha kwa mbali yaliweza kuyasikia mazungumzo yale. Mazungumzo ambayo
kadri nilivyokuwa nikiyasikia ndipo roho yangu ilianza kupambana na maumivu
makali, hakika roho ilikuwa ikiniuma mno kutoka na kile ambacho mjomba alikuwa
akizungumza. Yalinifanya kwa mara nyingine nivichukie viumbe vinavyoiitwa
wanawake hasirani kwa katika maisha yangu.
Nilinyanyuka pale nilipokuwa nimeketi,
si kutaka tena kuendelea kuyasikia yale, wakati huo mjomba alionekana myonge
sana. Unyonge ulikuwa ukichangiwa na kile ambacho alikuwa akisema kwa mama.
Hata nilipokuwa naingia ndani macho yangu yaliona wazi wazi hali ile.
Niliamua kujifungia mlango kimya ndani
ya chumba changu, taratibu nikienda kitanda, kitanda kikanipokea chenye
hakikuwa na hila kama wanadamu wengine, kilikubali kuupa faraja mwili wangu.
Mawazo nayo haya kuwa mbali, punde nilipojipunzisha ni kifakari maneno yale ya
mjomba nayo yakaona ni muda muafaka wa kunisurubu. Kweli yalifanikiwa, muda
mchache yalianza kunitoa machozi, hali iliyoniongezea hasira dhidi ya viumbe
vinavyoiitwa wanawake. Ni laani vikali, nadhani hata niliweza kumkufuru Mungu
kwa kwenda mbali zaidi, niliwatoa thamani kabisa viumbe hivyo, na hata kumweka
mama yangu katika aina nyingine ya jinsi na si jinsia ya viumbe hivyo, hakika
kichwa changu kilikuwa maji. Maji yalipoteza uelekeo na sasa yalikuwa yanaenda
sehemu isiyojulikana.
Baada ya muda kidogo, hasira
zilivunipungua ni kakumbuka bado nilikuwa na kazi ya kusoma kijitabu kile kilichoandikwa
na kaka katika miaka kadhaa iliyopita. Nikaishughulisha mikono yangu kupambana
kule nilipokuwa nimekiweka, hapakuwa pengine nilikuwa nimekihifadhi chini ya
godoro. Sekunde kadhaa mikono yangu
ilikuwa imekamata vizuri, ikiendelea kutafuta sehemu niliyokuwa nimeishia,
macho nayo bado yalikuwa katika ubora wake, yaliweza kuona vizuri maandishi yale.
*******
Siku kadhaa mbeleni jambo lile
linishinda kabisa kwa namna nilivyokuwa nikimpenda Irene katika maisha yangu,
iliniwia vigumu sana kusahau penzi lake. Kiukweli moyo wangu ulimpenda kweli,
hapo nikaanza kuikumbuka siku ambayo kwa mara ya kwanza nilipoonana nae. Si kujua Mungu anakusudio gani ndani ya
maisha yangu katika siku hiyo. Ilikuwa
kama siku nyingine ziendazo dunia lakini tofauti yake, akili yangu ilikuwa haikuwa
na mpango wa kutoka juu ya kitanda cha hostel nilipokuwa nimelalia. Ilitokana
na kimvua cha wastani kilichokuwa kimepiga siku nzima na kuleta kiubaridi ndani
ya jioni ya siku hiyo, hali ambayo ilinifanya niendelee kubiringita ndani ya
kitandaa. Lakini baada ya muda niliamua kujitoa eneo lile, nilijishangaa tu
hata wazo la kwenda cafe area linajia.
Hivyo baada ya kushindana na fikra
zangu nilijukuta miguu yangu inatoka ndani na kuongoza maeneo yale. Nilipofika
eneo lile niliingia na kuagiza chakula kama kawaida yangu, na kuelekea meza
ambayo mara nyingi huwa naitumiaga. Muda kidogo baada ya kukaa muhudu alileta
chakula nilichokiagiza.
Wakati naendelea kula walikuja wadada
kama watatu hivi karibu ilipokuwa meza yangu, na kuketi katika moja ya meza
ambayo haikuwa mbali na nilipoketi mimi. Sikuwajali kama kawaida yangu,
niliendelea kula. Kwa mbali nilikuwa nikiyasikia mazungumzo ya wadada wale.
Balaa lilikuja pale walipokuwa wakiendelea kuzungumza. Maana kuna sauti ya moja
kati ya wale wadada ilikuwa ikipenya sawia ndani ya ngoma za masikio yangu. Na
kuleta hali ya tofauti kidogo, hali ambayo kamwe sikuwahi kufikiria kama
ingeliniacha na maumivu makali ndani yake.
Hata sikujua sauti ile ilikuwa ina lengo gani pale mwanzoni maana kwasababu kupenya kwake ndani ya masikio yangu ilikuwa ukiupa moyo wangu faraja kwa muda mfupi. Nilijihisi kusisimuka sana ndani ya mwili wangu, msisimko ambao kwamwe sikutaka tamani uache kunisisimua tangia nilipoanza kuisikia. Ilinibidi nigeuke kuelekea sauti inapotokea hakika macho yangu hayakuamini kile nilichokuwa nikikiona, nadhani yalikuwa katika dhahama nyingine, ni hiyo dhahama ambayo imeghalimu maisha yangu kwa kiasi kikubwa.
Post a Comment