July 18
2016 Naibu Makamishna wa Polisi 25 na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa
Polisi 35 wamekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma, Ikulu
Jijini Dar es salaam.
Muda mfupi
baada ya kiapo hicho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli amewaagiza viongozi wa Jeshi la Polisi Tanzania kuwaondoa
watumishi wote wasiokuwa askari polisi na ambao wamekuwa wakijihusisha
na vitendo vya ukiukwaji wa taratibu na ufujaji wa fedha za umma ili
kulinda heshima, nidhamu na uadilifu ndani ya jeshi hilo, Rais Magufuli
amesema……
>>>’Mnajua
kupeleleza, mna vyombo vyote, ofisi ya IGP (Inspekta Jenerali wa
Polisi) ipo palepale, ofisi ya DCI (Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai) ipo palepale, Makamishna wote mnazunguka mnakwenda palepale,
mwizi mnae palepale, mnashindwa kumshika’
>>>”Kama
mnafikiri kuwa na raia katika jeshi la polisi wanawaharibia kazi zenu
hamisheni raia wote na wapelekeni utumishi, kwani hakuna mhasibu ambaye
ni askari polisi? hakuna mhandisi ambaye ni askari polisi? hakuna afisa
tawala ambaye ni askari polisi?
>>>‘Mimi
nafikiri kama matatizo ya wizi na wafanyakazi hewa yanaletwa na raia
waliomo ndani ya jeshi la polisi na majeshi yetu mengine, IGP
kaorodheshe raia wote wanafanya kazi Jeshi la Polisi ili waondolewe na
tuwapangie kazi nyingine uraiani’
Post a Comment