Maafisa wa
upelelezi nchini Marekani wamesema kuwa programu ya komputa inayotumiwa
na jopo linalosimamia kampeni ya Bi Hillary Clinton imedukuliwa.
Mameneja wanaosimamia kampeni ya Bi Clinton walisema kuwa wadukuzi hao wameingilia mawasiliano katika kompyuta hiyo.Awali kamati ya jopo hilo inayosimamia ukusanyaji pesa za kampeni ilisema kuwa mawasiliano yake yalikuwa yamedukuliwa.
Vyombo vya habari Marekani vinasema kuwa udukuzi huo huenda unahusika na shughuli za upelelezi za Urusi.
Juma lililopita mtandao wa kufichua habari za siri wa Wikileaks, unaodhaniwa kuwa na uhusiano mkubwa na Urusi ulifichua barua pepe nyingi kuhusiana na chama cha Democratic.
Post a Comment