Mara nyingi imezoeleka wachezaji kupata
umaarufu kutokana na kazi zao nzuri wanazofanya uwanjani na sio
vinginevyo, July 19 mtu wangu wa nguvu nimekutana na Top 5 ya mastaa wa
soka ambao ni maarufu sana mitandaoni kuliko uwanjani.
5- Jack Wilshere twitter
account yake inaonekana kuwa active kwa muda mwingi kiasi cha
kufanikiwa kupata follower milioni 1.24, Wilshere akaunti yake mara
nyingi anaweka picha zake za mazoezi, mechi, maisha binafsi na marafiki
lakini zimeonekana kupata retweet nyingi kutoka kwa mashabiki wake.
4- Mario Balotelli mshambuliaji wa kimataifa wa Italia ambaye kwa sasa amerudi katika klabu yake ya Liverpool akitokea AC Milan
kwa mkopo ni mmoja kati ya wachezaji wanaotajwa kuwa maarufu katika
mitandao ya kijamii kuliko uwanjani, kutokana na utovu wake wa nidhamu
amekuwa na headlines nyingi binafsi mitandaoni kuliko headlines za
uwanjani.
3- Joey Barton ambaye kwa sasa hayupo katika Ligi Kuu England nae hatofautiani sana na Mario Balotelli,
huyu nae ni maarufu mitandaoni kwa matukio ya kizembe na utukutu
uwanjani, kitu ambacho kimekuwa kikimfanya ajadiliwe mara kwa mara
mitandaoni kwa upande hasi kuliko kujadiliwa kwa mambo mazuri.
2- Emmanuel Adebayor amewahi kucheza baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya kama Arsenal, Man City, Real Madrid na Tottenham Hotspur,
anatajwa kama mmoja kati ya mastaa ambao wanapenda kutumia facebook na
twitter na ukilinganisha na matatizo yake na familia yake yaliokuwa
yakijadiliwa kupitia facebook kilimfanya awe maarufu zaidi mtandaoni.
1- Mchezaji wa kimataifa wa Ghana ambaye anaichezea klabu ya FC UFA ya Urusi Emmanuel Frimpong
amekuwa maarufu kwa sababu ya kuwa active sana twitter na kuwa na
rekodi ya kutweet 8k tweets, rekodi ambayo ni zaidi ya muda wake
alioonekana uwanjani, yaani ameonekana mtandaoni mara nyingi zaidi
kuliko uwanjani.
Post a Comment