Robert Mugabe
Rais wa Zimbabwe
Robert Mugabe amewaambia maseneta wa Marekani waliozuru taifa hilo
kwamba watajutia kutofanya urafiki naye iwapo Donald Trump atachaguliwa
kuwa rais katika uchaguzi wa mwezi Novemba.
Maseneta hao Chris
Coons na Adam Schiff waliambia gazeti la Politico nchini Marekani kwamba
walikuwa katika taifa hilo kuzungumzia kuhusu usafirishaji wa wanyama
mwitu na kwamba waliomba kukutana na rais huyo na wakashangaa kwamba
alikubali kuonana nao.Maseneta hao wamesema kuwa Mugabe aliwataka kuelezea kwa nini Marekani inaliwekea vikwazo taifa hilo ambapo walitoa sababu kadhaa.
Ni wakati huo ambapo bwana Mugabe aliwaambia: ''Wakati Trump atakapokuwa rais mutatamani mungefanya urafiki nami''.
Post a Comment