0

Mchezaji wa timu ya Likongowele city akipiga mpira


mchezaji wa Mpengele fc akitolewa nje mara baada ya kuchezewa vibaya
Mchezaji wa Likongowele city aliamaki akitaka mkupiga mchezaji wa timu ya Mpengele fc mwenye jezi namba 5
Baada ya mwamuzi wa mchezo kumpa kadi nyekundi mchazaji wa Timu ya Likongowele city na kukataa kutoka nje polisi waliingia uwanjani hali ikawa hivi jana
Baada ya mwamuzi wa mchezo kumpa kadi nyekundi mchazaji aliyesimama katikati wa Timu ya Likongowele city na kukataa kutoka nje polisi waliingia uwanjani hali ikawa hivi jana


Hatua ya Robo fainali ligi ya Liwale super cup ilianza jana julai 12 mchezo uliochezwa uwanja wa wilaya ya Liwale kulikuwa na mchezo mmoja kati ya Mpenfele fc dhidi ya Likongowele city.

Katika kipindi cha kwanza hadi dakika 45 zinamalizika hakuna timu hata mmoja ilioweza kufumania nyavu.
Kpindi cha pili namo dakika ya 46 Ikram Kigwalilo aliweza kuiandikia Likongowele city goli la kwanza lakini Likongowele city walionekana wakicheza wamerodhika na goli hilo.

Baada ya dakika 2 ikiwa dakika ya 48 Abubakari Ali aliweza kusawazisha goli hilo na dakika ya 73 Habibu Mutwe aliweza kuiandikia goli la pili Mpengele fc na kuamua kucheza kwa  kulinda lango lao na mpaka dakika 90 zinakamilika matokeo yalikuwa Mpengele fc 2-1 Likongowele city.

Leo julai 13 kutakuwa na mchezo mkali sana utakaowakutanisha wali wa wilaya kati ya HAWILI FC Vs KIGAMBONI FC mchezo utaochezwa kwenye uwanja wa wilaya ya Liwale majira ya saa 10 jioni.

Post a Comment

 
Top