Raia kote nchini Afghanistan
wanashiriki katika siku ya maombolezo, kufuatia shambulio la bomu la
mlipuaji wa kujitoa mhanga, lililofanyika jana Jumamosi katika mji mkuu
wa nchi hiyo-Kabul.
Watu themanini waliuwawa, huku zaidi ya 200 walijeruhiwa.Mlipuaji bomu alikuwa akiwalenga waandamanaji wa jamii ndogo ya Hazara - ambao wengi wao ni waislamu wa Ki-Shia.
Kundi la Islamic State - linachoshirikisha wapiganaji wenye msimamo mkali wa waisalmu wa Ki-Sunni- kimekiri kuhusika na shambulio hilo.
Rais wa Afghan, Ashraf Ghani, ameahidi kulipiza kisasi.
Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Afghanistan, umetaja shambulio hilo kama uhalifu wa kivita.
Post a Comment