Mahakama kuu nchini
Tanzania leo imeidhinisha umri halisi wa kuolewa kwa mtoto wa kike kuwa
miaka 18. Wasichana wenye umri wa miaka 14 huolewa kwa ridhaa ya wazazi
wao.
Mahakama kuu imetoa muda wa mwaka mmoja kuhakikisha kuwa
Serikali inasahihisha sheria ya mwaka 1971 kifungu cha 13 kinachoruhusu
Mtoto wa kike kuozwa akiwa na umri miaka 14
Wasichana wanaoolewa
katika umri huu mara nyingi wanakabiliwa na unyanyasaji wa majumbani
sambamba na kutengwa na jamii huku wakipewa nafasi ndogo kwa ajili ya
elimu na ajira.
Huu ni ushindi mkubwa kwa wanaharakati wa Tanzania
katika kupigania haki za watoto na sasa itakuwa rahisi kuwaokoa
wasichana wanaoathirika na utamaduni wa kuozeshwa wakiwa wadogo.
Uamuzi
huu umekuja wakati Bunge kupitisha sheria ya kifungo cha miaka 30 ama
faini ya dola 2500 kwa mwanaume atayebainika kumuoa ama kumpa mimba
mwanafunzi.Hata hivyo sheria hii inawatenga maelfu ya wasichana ambao si
wanafunzi.
Post a Comment