MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza kuanza rasmi
kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika mkoa huo ili kuhakikisha
wanafunzi wanasomea katika mazingira mazuri.
Makonda alitangaza kuanza kwa kampeni hiyo jana baada ya kupokea msaada wa mabati 10,000 yenye thamani ya Sh milioni 200 kutoka kwa umoja wa kampuni ya Motisun kupitia kampuni ya MMI Steel, kwa ajili ya kuezekea madarasa yatakayojengwa kwa fedha zilizotolewa na Rais John Magufuli.
Aidha, Makonda alipokea madawati 1,000 kutoka kwa taasisi ya Baps Charities ambayo alisema si tu yatamaliza changamoto ya sasa bali hata kwa miaka ijayo kama idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa itaongezeka.
Akizungumza wakati wa kupokea mabati hayo, Makonda alisema, kwa sasa ameanza kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo ameziomba kampuni na watu binafsi kujitokeza kusaidia ujenzi wa vyumba hivyo.
Alisema, Rais Magufuli alitoa Sh bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika mkoa wake, hivyo mabati hayo yatasaidia kuezeka madarasa yakayojengwa.
“Sasa natangaza rasmi kuanza kwa kampeni ya ujenzi wa madarasa, kwenye madawati bado tunaendelea, siwezi kusema yametosha. Mchango huu unaongeza nguvu si tu kwa kumaliza changamoto kwa sasa bali tunajipanga kwa ajili ya baadaye,” alisema Makonda.
Alisema suala la kuchangia madawati na ujenzi wa madarasa ulioanza ni hiari na upendo alionao mtu na kwamba kuna dhana imejengeka miongoni mwa watu kufikiri kampuni zinatoa misaada, zinatoa kwa ajili ya kupata upendeleo au zinakwepa kodi, jambo ambalo si kweli.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi mabati hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MMI Steel, Subhash Patel, alisema mabati hayo yana uwezo wa kuezeka madarasa 143 ambayo yana uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 6,000 kwa wastani wa wanafunzi 45 kila darasa.

Post a Comment