Msanii
huyu amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua Sekta ya Sanaa yeye
binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonesho yenye kukiuka
maadili. Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke
sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada
mbalimbali.
Ieleweke
kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23
ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kuhakikisha linalinda maadili
miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya
sanaa.
ikumbukwe
kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana
na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi
kubadilika na kuachana na tabia hiyo.
Kwa
hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho
kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na
wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama
kazi nyingine.
Kwa
sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa Pale Kati patamu ambao uko
mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu
yaani uchi wa mnyama.
Kwa
mantiki hii BASATA halitavumilia wasanii wachache ambao wanataka
kuigeuza tasnia ya sanaa na wasanii genge la wahuni wasio na staha na
wanaojipanga kuibomoa jamii. BASATA linapenda kueleza ya kufuatayo
• BASATA linatamka kuwa limeufungia wimbo huu rasmi kutumika kwa namna yoyote ile.
• Aidha pamoja na adhabu ya kufungia wimbo huu hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapotengeneza kazi zao.
SANAA NI KAZI, TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI.
Post a Comment