TUKIO la aina yake limefanywa kijana Andrew Muganda (26) aliyeripotiwa kumpiga mdogo yake Wycliffe Shitanda (23) hadi kumuua, kisa kikidaiwa kuwa alivaa nguo na kofia ya kaka yake huyo bila idhini yake, tukio lililotokea hivi karibuni katika Kijiji cha Shamberere, Malava, Kakamega nchini Kenya.
Tarifa iliyotolewa na mama yao mzazi, Violet Lagu, inasema Muganda alimuuliza mdogo wake kwa nini alivaa nguo zake bila idhini yake naye mdogo mtu akajibu kwa jeuri.
“Nina taarifa zako kuwa umekuwa ukitafuta ugomvi na mimi,” Shitanda alimjibu kaka yake. Papo hapo wawili hao walianza kupigana jambo lililopelekea Muganda kumdhibiti mdogo wake Shitanda kwa kipigo kikali hadi kupoteza maisha yake.
Lagu alisema msiba huo umeleta simanzi kubwa ndani ya familia yao kwani walikuwa kwenye maandalizi ya mazishi ya mama mkwe wake ambaye alifariki siku za usoni.
“Tupo njia panda na hatujui tupange vipi mazishi ya watu wawili. Tunaomba msaada kwa mtu yeyote atakayeweza kutusaidia maana mpaka sasa mwili wa mama bado upo mochwari kwa kukosa pesa.” Alisema Langu.
Vyombo vya usalama mjini Kakamega vimelaani tukio hilo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Maghaibi, Moses Ombati amesema tayari jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa mtuhumiwa wa kosa hilo na anaendelea kuhojiwa na pindi upelelezi utakapokamilika atapandishwa kizimbani kujibu tuhuma zinazomkabili.
CHANZO: Standard
Post a Comment