Jeshi
la Polis kanda Maalumu jijini Dar es salaam limekamata watuhumiwa sugu
1,065 kwa makosa mbalimbali yakiwemo unyang’anyi wa kutumia nguvu, wizi
wa maungoni, wapiga debe, wavuta bangi, kikosi cha mbwa mwitu,
watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti tofauti katika maeneo
mbalimbali jijini Dar es salaam.
Hayo
yamesemwa na kamishina wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Simon
Sirro alipokua akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo, Sirro
alisema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumekuja baada ya kufanya
operesheni kali katika maeneo mbalimbali jijini humo.
Aidha
pamoja na kufanikisha zoezi hilo kwa watuhumiwa hao,jeshi hilo pia
wamekamata lita 952 za pombe aina ya gongo,bangi puli 227, kete 210, na
misokoto144 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Katika
hatua nyingine ,kikosi cha kupambana na wizi wa simu cha polisi
kimefanikiwa kuwatia hatiani watuhumiwa watatu(3) kwa makosa ya uporaji
wa simu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa kinondoni,watuhumiwa hao ni
Richard Augustino (18), Abdallah Chande (36),Abdallah Said (22) wote
wakazi wa jijini Dar es salaam.
Hata
hivyo kamanda Sirro aligusia zoezi zima la uhakiki wa silaha na kusema
kuwa lilienda vizuri na watu walijitokeza kwa wingi japo kuna
changamoto kadhaa zilizojitokeza
Kamanda
Sirro amesema idadi ya watu waliojitokeza kuhakiki silaha kwa wilaya
zote tatu ni 11,602 na jumla ya silaha 14107 zilihakikiwa.
Pia
kasema Jumla ya silaha 66 zilisalimishwa kutokana sababu mbalimbali
ikiwamo mmiliki wa silaha kuwa na umri mkubwa na kushindwa kumudu
silaha. Zoezi la uhakiki wa silaha limeiingizia Serikali mapato kiasi
cha Mil 198.8
Jeshi
hilo kupitia kikosi cha usalama barabarani kanda maalumu ya Dar es
salaam limeweza kujikusanyia kiasi cha shilingi 562,860,000/= kutokana
na ukamataji wa makossa mbalimbali ya usalama barabarani kuanzia tar
15/7/2016 hadi 21/7/2016.
- Idadi Ya Pikipiki Zilizokamatwa -1,413
- Idadi Ya Magari Yaliyokamatwa –17,349
- Daladala Zilizokamatwa -7220
- Magari Mengine (Binafsi Na Malori)- 10,129
- Jumla Ya Makosa Yaliyokamtw- 18,762
6. Bodaboda Waliofikishwa Mahakamani Kwa Makosa Ya Kutovaa Helmet Na Kupakia Mishkaki ni 49
Post a Comment