
Mojawapo ya swali kubwa ambalo watu wengi wanajiuliza kila mara ni
kuwa, ni hatua gani muhimu anayoweza mtu yoyote kuichukua ili kuweza
kufikia katika eneo la kutengeneza mafanikio yake? Hii inaonyesha ni
jinsi gani watu wengi wanavyojaribu kutafuta njia yoyote ya kufanikiwa
kwa gharama yoyote ile hata kama ni kwa njia ya mkato ilimradi kufikia
katika mafanikio, na kumbuka mafanikio ya kweli hayana njia ya mkato.
Kadiri unavyochukua hatua ya kivitendo pasipo uoga, ndio kadiri
unavyozidi kuongeza nafasi ya kwenda katika mafanikio unayoyahitaji.
Nidhamu yako, uwezo wa kutokubadilika badilika katika kufaata maamuzi
yako na kutokukata tamaa katika hatua uliyoamua kuichukua katika
kufuata ndoto yako, hizi ndio tabia pekee zinazoweza kukujengea
kujiamini na kufanikiwa haraka ukiunganisha na mambo mengine bora
unayoweza kuyatumia katika kufanikisha ndoto na malengo yako uliyonayo
katika maisha.
Ni vizuri ufahamu ni namna gani ya kuchambua na kupigia hesabu kamili
ya kiasi gani cha muda na hatua maalum unazotakiwa kuzichukua ili
kujenga mawazo mapya, kujiamini na kuvumbua mambo mapya yatakayokusaidia
katika kutengeneza mipango yako mizuri ya kufikia katika mafanikio
makubwa.
Watu wengi wanafeli na kushindwa kabisa ni kwa sababu wanashindwa
kuchukua hatua sahihi zinazoweza kuwapeleka katika kuchukua vitendo
timilifu vya kuwapeleka katika mafanikio yao. Unapohitaji kuchukua hatua
za kivitendo katika jambo lolote lile la mafanikio ni uamuzi wa kwako
kufanya uchaguzi katika nganzi hizi nne.
1: Kutokuamua kufanya chochote au kutokuamua kuchukua hatua kabisa.
Si uongo kwamba kuchukua hatua ya kivitendo ndio jambo pekee
linaloweza kuwa chachu ya mtu yoyote kufanikiwa katika malengo na
mipango yake aliyonayo. Uamuzi wa kuchukua hatua au kutokuchukua hatua
katika kufuata njia yako ya mafanikio upo juu yako tofauti na
unavyofikiri, wewe ndiye mwenye uamuzi wa mwisho juu ya kufanikisha
ndoto yako. Watu wengi ambao wameshindwa kuona matokeo yoyote katika
taaluma zao, biashara, mahusiano, nakadhalika, hii ni kwa sababu wengi
wao si watu wa kuchukua hatua zinazostahiri kwa ajili ya kufikia ndoto
zao nzuri walizonazo.
Yawezekana ni mmojawapo wa watu wenye kupanga malengo na mipango
mingi ya kufikia ndoto yako, lakini si mtu uliye mwepesi wa kuchukua
hatua ya juu za kivitendo, nataka nikuambie ni ngumu sana kufanikiwa na
kufikia hatima ya ndoto yako. Kutokuamua kufanya chochote juu ya mipango
na malengo yako uliyonayo ni uamuzi ulio ndani yako binafsi na mwenye
uwezo wa kuubadili wewe pekee. Uamua kubadilika na kukimbia uamuzi huu
husio mzuri wa kutokuchukua hatua za kivitendo kabisa katika malengo na
mipnago yako mizuri uliyonayo.
2: Kuamua kurudi nyuma.
Mara nyingi hatua hii hutokea pale mtu anapojaribu kutimiza malengo
au jambo fulani lenye mafanikio kwake binafsi na pale linapotokea jambo
gumu au zito mbele yake kama changamoto uamua kurudi nyuma au kukata
tamaa au kukimbia tatizo badala ya kulikabili. Mtu huyu ninaweza kumwita
ni mtu aliye mwoga wa kukabili changamoto, huku pasipo kujua kupitia
changamoto huwezi kufikia kufanikiwa kwa kiwango unachokitaka.
Watu wengi wanaorudi nyuma kwa ajli kutimiza ndoto zao kwa uoga wa
jambo fulani linalowakabili mara nyingi huwa ni watu wa kutoa visingizio
juu ya hatua waliyoamua kuichukua ya kurudi kwao nyuma. Ni watu
wanaotumia muda mwingi kutoa sababu juu ya kwa nini hatua waliyoichukua
na kwa nini wameamua kurudi nyuma kufanya jambo fulani. Nakusihi husiwe
miongoni mwa watu wanaotoa sababu na watu wanaorudi nyuma mara kwa mara
kwa sababu ya uoga bali amua kwenda mbele kwa ajili ya kufikia ndoto na
maono yako.
3: Kuchukua hatua ya kiwango cha kawaida au kati.
Watu wengi walioamua kuchukua kiwango cha kawaida cha kutimiza
malengo na mipango yao waliyonayo, watu hawa kwa idadi yao ni wengi na
tena ni kubwa sana katika jamii yetu ya leo. Hili ni kundi la watu
ambalo kwa makusudi kabisa au kwa kutokujua limeamua kujikita kuchukua
hatua za kivitendo kwa kiwango cha kati au kawaida tena wakati mwingine
kwa kujiurumia binafsi tofauti na ndoto zao zinavyowataka. Huwezi
kufanikiwa kwa kiwango cha juu, huku unachukua uamuzi wa kivitendo wa
nganzi ya chini au kawaida, kwamwe hutoweza kufikia mafanikio makubwa
unayoyataka.
Mara nyingi kundi la aina hii la watu ndio linalotengeneza maisha ya
watu wenye uchumi wa kati (middle class people) katika jamii
inayotuzunguka, watu hawa ndio wenye maisha ya kawaida katika ndoa,
taaluma, mafanikio kifedha, nakadhalika; watu hawa hawafanikiwi zaidi
kwa sababu si watu wenye kujituma zaidi na kuongeza bidii fulani katika
kujiletea mafanikio yao halisi na ya kweli ambayo hata Mungu
ameyakusudia juu yao. Usikubali kuishi maisha ya chini ya kiwango chako
cha mafanikio hasa kwa kutenda mambo kwa namna ya kawaida, ongeza bidii
ili ufikie hatua ya juu ya mafanikio yako.
4: Kuchukua hatua ya kiwango cha juu kabisa.
Hii ndio hatua ya juu ambayo kila mtu anatakiwa kuichukua katika
kutimiliza malengo na mipango yake ili kuweza kufikia ndoto na maono
yake aliyonayo. Angalia kwa mfano maisha ya watoto wadogo
waliokuzunguka, mtoto yoyote mdogo huwa anatenda au kuchukua hatua ya
kufanya vitendo vya hatari tena vikubwa ambavyo vinaweza kuwa hatarishi
kwake, lakini kama hasipopata mtu wa kumwambia basi uendelea kufanya
kitendo hicho. Hata mimi nakumbuka nikiwa mdogo kama miaka 7 hadi 10,
nilikuwa katika hali ya namna hiyo, ni kwa nini? Ni kwa sababu mtoto
mdogo hajui ubaya wa jambo lolote analolifanya; ila sasa ni kwa nini
afanye vitendo vikubwa vya namna hiyo na huo ujasiri unatufundisha nini
kwetu sisi kama watu wazima?
Nataka nikuambie kuchukua hatua ya kivitendo kwa kiwango cha juu
kunahitaji ujasiri wa hali ya juu ili uweze kufanikiwa, kwa kuwa wengi
wameogopa kutenda mambo makubwa kwa hofu ya kuumia, kuabika, kupoteza
fedha, kupoteza heshima, nakadhalika. Lakini nataka ufahamu kuwa uamuzi
wa kuchukua hatua hii kwa uaminifu ili kuyafaata mafanikio yako na
kuifikia ndoto yako ni jambo bora zaidi kuliko kubaki katika hatua
nyingine nilizotoka kuzielezea hapo juu.
Watu hawawezi kufahamu kipaji na uwezo wako ulionao kama hautoamua
kuchukua hatua ya kivitendo ya kiwango cha juu tena kwa bidii ili
kuwafikia watu wengi kwa namna chanya ambayo itawagusa watu hao kwa
stahiri ya ajabu na wengi kukufahamu au kukutafuta kwa ajili ya kupata
msaada kutoka kwako. Kama ni kampuni haiwezi kuwafikia wateja wengi kwa
bidhaa na huduma zake kama haitohakikisha inatoa nguvu ya ziada ya
kuchukua hatua ya juu ya kivitendo kwa ajili ya kufanikisha malengo na
mikakati yake.
Hatua hii ya nne ndio imezaa mamilionea na mabilionea wengi unaowaona
leo hii katika dunia, unasubiri nini kwako wewe na mimi kuwa katika
hatua hii na kuchukua hatua ya kivitendo vya viwango vya juu ili kuwa
sehemu ya mafanikio makubwa kama wengine. Nakuambia inawezakana
kufanikiwa na mimi nimeanza muda kutekeleza hatua hii na sasa nakula
matunda yake na bado sichoki kuchukua hatua hii hadi niifikie ndoto
yangu ya kweli. Amua nawe kuwa miong
Post a Comment