0

Askari wa Burundi
Askari wa Burundi wakipiga doria katika mitaa ya Bujumbura, baada ya shambulio la guruneti, Februari 3, 2016.
Na Mwandishi Wetu, Burundi
Watu wasiopungua watano kutoka familia moja wameuawa kwa kuchomwa moto wakiwa hai katika kijiji cha Bucana, Wilayani Gitobe, mkoani Kirundo, kaskazini mwa Burundi.

Kwa mujibu wa Mshauri wa Mkuu wa wilaya Gitobe, wahanga kabla ya kuchomwa moto na kuteketea ndani ya nyumba yao, walichomwa visu.

Afisa huyo ameongeza kwamba idadi ya watu walioteketea kwa moto inaweza kuwa kubwa zaidi: "inasadikiwa kuwa kuna watoto ambao walikua ndani ya nyumba hiyo, ambao hawakupatikana, kutokana na moto mkali ambao ulikua ukiwaka, " amesema Mshauri wa Mkuu wa Wilaya ya Gitobe.

Visa vya mauaji vimekithiri katika nchi hiyo ndogo ya Afrika ya Kati. Burundi ni nchi ya Ukanda wa Maziwa Makuu ambayo imeathirika na mauaji, hasa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe viliyodumu zaidi ya mwongo mmoja, baada ya kuuawa kwa rais wa kwanza kutoka kabila la Wahutu, Melchior Ndadaye aliyechaguliwa mwaka 1993 kuliongoza taifa hilo, ambalo kwa miaka zaidi ya 60 lilikua likiongozwa na kabila moja tu ya Watutsi.

Mashirika yanayotetea haki za binadamu yanabaini kwamba watu zaidi ya 270,000 wamelazimika kuyahama makazi yao na kukimbilia katika nchi jirani na Ulaya kwa kuhofia maisha yao, na wengine waliosalia nchini humo wameendelea kushuhudia visa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mauaji, uporaji, unyanyasaji, ... Mashrika hayo yameendelea kuishtumu serikali kuhusika na visa vyote hivyo vinavyoendelea kushuhudiwa nchini humo.

Hata hivyo Serikali imetupilia mbali tuhuma hizo, ikisema kwamba mashirika hayo ndio yamekua yakichochea chuki na mauaji ili yaweze kufikia madaraka.

Post a Comment

 
Top