Wanafunzi 7,802 waliosimamishwa masomo Chuo Kikuu Cha Dodoma wameiomba serikali kuwatizama upya na kuwawezesha kumalizia masomo yao hasa wale wenye vigezo vinavyostahili.
Hayo yamesemwa katika mkutano maalumu ulioitishwa na Mtandao wa Wanafunzi Nchini (TSNP) ambapo mtandao huo umempongeza Rais Dkt. John Magufuli na serikali yake kwa hatua iliyochukua kwa waliodahili wanafunzi wasio na vigezo.
Akitoa taarifa maalumu kwa niaba ya wenzake waliosimamishwa masomo, Mwanafunzi Gibson Johnson amesema kwamba wanaiomba serikali iwatizame kwa upya hasa wale ambao wana vigezo vya division 1, 11, na 111 kuweza kuendelea na masomo yao huku wenye alama za chini ya hapo wakitafutiwa namna nyingine.
“Tunaiomba na kuililia serikali iangalie wale wenye division I, II na III ituache tumalizie masomo yetu, lakini watakaokuwa na ufaulu wa chini kuanzia division IV itafute namna ya kuwasaidia,” amesema Johnson.
Aidha Katibu Mkuu wa Mtandao wa wanafunzi nchini Alphonce Lusako amesema TSNP inaiomba serikali kuwaruhusu wanafunzi ambao wamebakiza mwaka mmoja wa kumaliza masomo yao ya Stashahada (Diploma) waendelee na masomo yao.
Post a Comment