0
 mchezo wa fainali kati ya timu ya Bodaboda fc na Wakaanga sumu mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano hii leo
 Mashabiki wa soka waliokuja kuangalia mchezo wakifuatilia kwa umakini mchezo huu
Mgeni rasimi wa fainali ya leo Bw.Hassani Mpako akitoa nasaa kwa wachezaji na mashabiki wa soka
 Kikosi cha timu ya Wakaanga sumu wakisubiri kukabidhiwa mbozi wako mara baada ya kuiburuza bodaboda goli 2 kwa 1
 Mgeni rasimi akimkabidhi mwamuzi wa mchezo wa leo zawadi ya shilingi 20000 kwa kuonesha udhalendo wake wa kuchezesha michezo yote ya ligi
Mgeni rasimi bw.Hassani Mpako akikabizi mbuzi  kwa timu ya    Wakaanga Sumu ambao ni washindi wa ligi ya mbuzi vijana cup(picha na Mwamndae Mchungulike)

Leo ikiwa juni 5 katika ligi ya mbuzi vijana cup kulikuwa fainali kati ya timu ya Wakaanga sumu Vs Bodaboda mchezo uliotimua vumbi katika uwanja wa shule ya msingi Muungano wilayani Liwale Mkoani Lindi.

Magoli ya timu ya Wakaanga sumu yalifungwa namo dakika ya 9 na 76 goli yote yaliyofungwa na Mantu Hatibu huku goli la timu ya Bodaboda fc likifungwa namo dakika  ya 35 kupitia kwa mchezaji wao Saidi Milasi.

Katika mchezo huo kocha wa Bodaboda fc,Ridhiki Mbwani amekili kufungwa na ameyakubali matokeo ya jana pia alitoa ushauri kwa ligi zijazo kurekebisha kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza kwa ligi ya mbuzi vujana cup

Kocha wa Wakaanga Sumu, Saidi Matongo alisema amefurahishwa na ushindi alioupata richa ya kuwa na upinzani mkubwa kwa timu zote zilizoshiriki katika ligi hii na alibaini siri ya ushindi alioupata ni mazoezi na nidhamu kwa ujumla.

Richa ya kumalizika kwa ligi ya mbuzi vijana cup mzamini wa ligi hii Bw. Haji Mtutuma alisema  katika upande wa mchezo wa mpira wa miguu wilayani Liwale mkoani Lindi kuna changamoto kubwa ya kukosefu wa waamuzi wa kuchezesha mpira.


Katika fainali mgeni rasimi alikuwa Bw. Hassani Mpako aliweza kukabizi zawaidi ya kombe la mbuzi kwa washindi na kila timu zilishiriki 12 zilijipatia kifuta jasho kwa kila timu shilingi 20000/= pia alitumia nafasi hiyo kuambia vijana kupenda michezo kwakuwa michezo ni moja ya ajira kama watakuwa wanacheza vizuri na kuwa na nidhamu na aliongeza kusema timu zijipange kwa Ligi nyingine inayotarajia kufanyika mwezi ujao.

Post a Comment

 
Top