0


Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba iliyoko mkoani Kagera itaanza zoezi la kubomoa nyumba zote zilizoko  ndani ya mita 60 toka kwenye vyanzo vya maji ambavyo ni pamoja na mito na ufukwe wa ziwa victoria zilizojengwa baada sheria iliyopitishwa na bunge  mwaka 2003 ya kuzuia ujenzi wa nyumba katika maeneo hayo.

Hayo yameelezwa na Katibu tawala wa wilaya ya Bukoba, Clement Ndyamkama  kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bukoba, Jackson Msome wakati wa  ukielezea mikakati ya wilaya hiyo ya uhifadhi wa mazingira wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo katika Manispaa ya Bukoba yalifanyika  katika kata ya Nshambya amewataka wale wote waliojenga nyumba  ndani ya mita 60 toka kwenye vyanzo vya maji na ufukwe baada ya kupitishwa sheria hiyo wazibomoe  kwa hiari yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya Manispaa ya Bukoba, Wallace Karia amesema waliojenga nyumba ndani ya mita 60 toka kwenye vyanzo vya maji kabla ya kupitishwa sheria ya mazingira ya mwaka 2003 wataondolewa kwenye maeneo hayo na watalipwa fidia hivyo akawataka wasifanye mwendelezo wa ujenzi wa nyumba hizo ili wasiziongeze thamani.

Naye, Frederick Linga afisa afya na mazingira wa Manispaa ya Bukoba amesema Manispaa hiyo itahakikisha inalinda na kuhifadhi mazingira na kuwashughulikia wale wote wanaofanya shughuli za kibinadamu ambazo ni pamoja na kilimo karibu na vyanzo vya maji, huku Justus Alexander mmoja wa wananchi akielezea macho yanayochangia vitendo vya uchafuzi wa mazingira na ujenzi holela karibu na vyanzo vya maji.

Post a Comment

 
Top