Mchakato wa mradi wa ujenzi wa bomba la
kusafirisha mafuta ghafi na safi kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga
sawa na umbali wa kilomita 1443 umeanza baada ya wadau watakaohusika na
mradi huo utakaogharimu zaidi ya dola za kimarekani bil 3.5 kuanza
kuweka utaratibu wa ulipaji wa fidia katika maeneo ambayo bomba litapita
pamoja na ujenzi wa gati kubwa katika eneo la Chongoleani lililopo
katika bahari ya Hindi.
Akizungumza katika mahojiano maalum
wakati wadau wa mpango wa bomba la mafuta walipotembelea eneo ambalo
Rais wa Uganda Yoweri Museveni na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe
Magufuli wataweka jiwe la msingi hivi karibuni.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la maendeleo ya Petrol nchini Dkt. James
Matalagio amesema hivi sasa wapo katika utaratibu wa kuunda kampuni
itakayosimamia uingizaji wa mafuta kabla ya ujenzi wa gati kuanza.
Kwa upande wake Afisa mipango mkuu
miradi binafsi na ya kitaifa wa mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini
Alfred Mantutela amesema wameomba wajenge ghati kwa gharama zao pamoja
na kuhudumia meli zitakazokwenda kuchukua mafuta ghafi na safi katika
bandari ya Tanga.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Martini Shigella pamoja na wakazi watakaohusika na zoezi la ulipwaji wa
fidia katika mashamba yao na nyumba zilizopo eneo la Chongoleani
wamesema kuwa wamejipanga katika kuhakikisha kuwa zoezi hilo
linafanikiwa.
Post a Comment