0
Profesa Joyce Ndalichako 
Ripoti ya uchunguzi wa kamati iliyoundwa na Waziri Elimu wa Tanzania Profesa Joyce Ndalichako imeibua ufisadi katika bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini Tanzania.

Ufisadi huo ni pamoja na bodi kutoa mikopo isiyojulikana kwa wanafunzi zaidi 2000 wa kiasi cha shilingi bilion 14 za Tanzania sawa na dola milioni 7 za marekani.

Kamati hiyo iliundwa baada ya kusimamishwa kwa watendaji wakuu wa bodi hiyo.
Aidha bodi hiyo imegundua upotevu wa Zaidi ya dola Milioni 1.3 zilizolipwa kwa wanafunzi wa vyuo kadhaa ambazo hazitambuliwi na vyuo hivyo huku fedha hizo zikiwa hazijarudishwa.

Waziri huyo amesema kuwa baada ya kuyabaini mambo hayo,serikali serikali imechukua hatua za kutoa wiki mbili kwa bodi ya mikopo kuwachukulia hatua mara moja wote wanaohusika ikiwemo watumishi waliosimamishwa.

February mwaka huu waziri huyo aliwasimamisha kazi baadhi ya watendaji wakuu wa bodi hiyo baada ya kubaini udhaifu katika utekelezaji wa majukumu yake ambapo pia ameagiza uchungu ufanyike

Post a Comment

 
Top