Mwandaaji
maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini,Godfrey Kunambi maarufu kama
"Mantano" amewataka wasanii kutoka sehemu mbalimbali nchini kujitokeza
katika usahili kwa ajili ya kujiunga na lebo yake ili kuleta chachu ya
ubora wa muziki na wasanii nchini.
Akizungumza na mwandishi wetu
producer mantano alisema ameamua kufanya usahili kwa ajili ya wasanii
watakokuwa chini ya studio yake na kuandaliwa katika nyanya zote
kimuziki na kimaisha.
"Muziki ni kazi na vijana wengi hawana
kazi nchini na wanavipaji,kwa hiyo tumeanzisha lebo ambayo watakuja
wasanii na kufanya usahili atakayefanikiwa kupita atakuwa chini ya
studio na kurejodewa nyimbo,malazi,chakula na kutangazwa zaidi katika
vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi".Alisema Mantano.
Mantano
ambaye ni muandaaji wa muziki katika studio mpya zijulikanazo kama Good
Music Record iliyopo Kinondoni Dar es salaam amewahi kufanya kazi
katika studio mbalimbali kubwa nchini zikiwemo,Rocka tz ya
morogoro,Dhahabu Record,Baucha Record, kazi kwanza na studio kibao
nchini.
Aidha Producer huyo aliyewaki kufanya ngoma kaili
zilizotamba zikiwemo Ukoje naye ya K One na Maunda Zorro na Baghdad
aliyomshilikisha chibwa inatwa TIP TIP alisema usahili huo ulianz
kufanyika studioni hapo kuanzia june 5 mwaka huu mpaka julai.
Vile
vile producrec huyo alitoa mawasiliano ya jinsi ya kufika kwenye
usahili ambayo ni 0656 094194 au 0716 000170 ambazo wasanii mbalimbali
wanaotaka usahili watawasiliana kupitia namba hizo.
Post a Comment