0

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara
Jeshi la polisi mkoani Mtwara limeomba Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kuelekeza nguvu kwenye eneo la usajili wa laini za simu ambalo limeonyesha kuwa na changamogo nyingi ikiwemo taarifa zisizo sahihi zinazochangia jeshi hilo kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo mara zinapotokea taarifa za uhalifu ama kumtusi mtu kupitia simu ya kiganjani.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Henry Mwaibambe wakati akichangia maoni yake katika mafunzo ya kuelezea nia njema ya serikali ya kuzifungua simu feki hapa nchini zoezi ambalo linatarajiwa kufanyika majira ya saa sita usiku wa leo.

Amesema Jeshi la Polisi nchini limekuwa likipata wakati mgumu katika kufanya upelelezi wake mara wanapopata kesi zinazohusiana na wizi wa pesa kupitia simu ama kudhalilishwa kwa mtu wanapofuatilia taarifa za mhalifu kwenye simu yake mara nyingi wanasajili majina ya uongo na vitambulisho visivyo sahihi na hivyo kushindwa kufanikiwa kiutendaji.

Kufuatia hali hiyo wameiomba TCRA kupitia zoezi wanalolifanya kuhakikisha kipengele hicho kinaondolewa ukakasi ili kuliwezesha jeshi la polisi kutekeleza sheria hiyo ambayo nia yake ni njema kwa wananchi.

Post a Comment

 
Top