0

MAAJABU YA STAFELI
TUNDA la stafeli linatibu magonjwa kadhaa, ikiwamo saratani kwa ubora wa karibu mara 10,000 ya matibabu ya kawaida yanayopatikana kwenye vituo vya afya, utafiti umebaini. Utafiti huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dawa cha Purdue nchini Marekani, umeeleza kuwa mbali na kutibu saratani, tunda hilo pia ni tiba ya matatizo ya

Msongo na mfadhaiko.
“Maajabu ya stafeli ni kwamba lina uwezo wa kuangamiza chembehai zenye saratani pasipo kusababisha madhara katika

mwili kama zinavyofanya dawa nyingine za ugonjwa huo au mionzi,” imesema sehemu ya utafiti huo uliochapishwa kwa mara ya kwanza katika Jarida la Kemia na Madawa la nchini

Marekani, mwaka 2010. Taasisi ya utafiti wa Saratani ya Nchini Uingereza(NIR) ilifanya utafiti wa kwanza kuhusu

Maajabu ya stafeli mwaka 1976. Katika utafiti huo ilibainika kuwa majani, mizizi na tunda la stafeli, vina uwezo wa kutibu saratani lakini matokeo ya utafiti huo hayakutangazwa kwa umma

kwa hofu ya kuua viwanda vya dawa za saratani. Inaelezwa kuwa kirutubisho kilichopo katika stafeli kinatumia jina la kibiashara la ‘Triamazon’ na kimepigwa marufuku kutumika nchini

Uingereza na Marekani kutokana na uwezo wake mkubwa wa kitiba. Utafiti mwingine uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kikatoliki nchini Korea na kuchapishwa katika jarida la Bidhaa Asilia ulibaini kuwa stafeli lina uwezo wa

kuponya saratani ya tumbo. Utafiti wa chuo hicho ulienda mbali na kusema kuwa tunda hilo linaweza kulenga seli za saratani tu, bila kushambulia seli muhimu za mwili kama ambavyo tiba ya

mionzi ifanyavyo. 
Tunda la Stafeli lina kirutubisho muhimu kiitwacho Annona Muricata, ambacho ndicho chenye uwezo wa kupigana na maradhi

ya saratani. Imeelezwa kuwa stafeli lina uwezo wa kutibu aina 12 za saratani ikiwemo ya matiti, kongosho, mapafu na ya kibofu cha mkojo. Pamoja na kutibu saratani,

kirutubisho hicho kilichopo katika tunda hilo pia huweza kutibu vimelea, shinikizo la damu, msongo wa mawazo, matatizo ya

mfumo wa fahamu na sukari.
Utafiti huo unaonyesha kuwa kirutubisho kimegwacho katika tunda hilo kinaweza kwa asilimia kubwa kupambana na saratani bila kumuacha mgonjwa na madhara kama kusikia kichefuchefu, kutapika, kupungua uzito na kunyonyoka nywele.

Post a Comment

 
Top