Licha ya Yanga kutangaza kuwa mchezo huo utakuwa ni bure ambapo
unatarajia kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Ofisa Habari wa Yanga,
Jerry Muro amesema tayari wameshapokea tarifa kutoka kwa wapinzani wao
hao kuwa watakuwa na mashabiki zaidi ya mia tano kutoka nchini DR Congo
kwa ajili ya kuisapoti timu yao.
Kuelekea katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa kesho
Jumanne saa 10:00 jioni, uongozi wa Klabu ya Yanga umesema kuwa
wanatarajia kuwapokea zaidi ya mashabiki mia tano wa TP Mazembe ambao
watakuwepo uwanjani kuishangilia timu yao.
“Tumepokea taarifa kutoka kwa wenzetu wa TP Mazembe ambao wametueleza
kuwa kuna msafara mashabiki wao wapatao mia tano wapo njiani, wanakuja
kwa ajili ya kuisapoti timu yao katika mchezo wa kesho,” alisema Muro na
kuongeza:
“Sasa niwaombe tu mashabiki wa Yanga na Watanzania kwa jumla
wajitokeze kwa wingi uwanjani ili tuwazidi hao wa kwao mia tano.”
Mashabiki wa TP Mazembe wanajulikana kwa kuwa na nguvu kubwa ya
kushangilia bila kujali wakiwa nyumbani au ugenini, ambapo walipowahi
kuja nchini miaka kadhaa iliyopita kucheza dhidi ya Simba walikuwa na
kikundi cha ngoma kilichokuwa kivutio kwa mashabiki wengi nchini.
Post a Comment