MKUU wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda
amesema kuanzia wiki ijayo tatizo la sukari litakuwa historia, kwani
viwanda vya sukari vya ndani vinaanza uzalishaji.
Ntibenda alisema hayo jijini hapa
wakati akikabidhi mradi wa ufugaji kuku wa kienyeji na mbuzi wa maziwa
katika Kata ya Muriet eneo la Kwamrombo, unaoendeshwa na Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF).
“Hivi sasa wananchi mnauziwa sukari
kilo moja kwa shilingi 2,500 hadi Sh 3,500 kwa kilo moja, lakini sasa
tunasema sukari itapatikana kuanzia wiki ijayo na wanaofunga Ramadhan
wasiwe na shaka, watapata sukari,” alisema.
Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro
alisema anaungana na serikali kuhakikisha maendeleo ya jiji la Arusha
yanapatikana, ikiwemo ukusanyaji wa kodi za majengo.
Post a Comment