Bodi mpya ya shirika la umeme Tanzania
– Tanesco imetakiwa kujikita zaidi katika kutafuta namna ya kuongeza
mapato ya shirika hilo ili liweze kujiendesha badala ya kutegemea fedha
kutoka serikali na kusababisha kukwama kwa baadhi ya miradi.Wito
huo umetolewa jijini Dar es salaam na katibu mkuu wizara ya nishati na
madini prof.Justine Ntalikwa wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo ambapo
ameiambia kuwa zipo changamoto nyingi zinazolikabili shirika hilo
ikiwemo kuelemewa na madeni ambayo kwa asilimia kubwa yamesababishwa na
mikataba ya dharula ambayo ilitokana na nchi kupungukiiwa na nishati ya
umeme.
Prof.Ntalikwa amebainisha kuwa kwa sasa
serikali inatekeleza mkakati wa kurekebisha sekta ya umeme ili kuifanya
Tanesco ijitegemee huku serikali ikiendelea kushirikiana nayo katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uunganishwaji wa huduma hiyo katika
maeneo ya pembezoni, na kusema kuwa changamoto inayobaki kwa tanesco ni
kutekeleza majukumu yao kwa wakati.
Post a Comment