June 19
2016, Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia na watoto ilitoa
taarifa kuhusu kuwepo kwa ugonjwa usiofahamika katika wilaya za Chemba
na Kondoa, mkoani Dodoma ambapo wakati huo kulikuwa na jumla ya wagonjwa
21 na vifo 7.
June
25 2016 Waziri Ummy Mwalimu ametoa taarifa kwamba idadi ya wagonjwa
imefikia 32 na idadi ya vifo imebakia 7 hii ni baada ya kuongezeka kwa
wagonjwa 11 katika kipindi cha wiki moja.
Waziri
Mwalimu amesema Wizara ifanya jitihda mbalimbali za kutambua kiini cha
ugonjwa huo baada ya kupeleka jopo la wataalamu ili kufanya uchunguzi wa
kina pia ameeleza kuhusu sampuli zilizofanyiwa utafiti…….
>>>’Sampuli
mbalimbali zikiwemo, haja ndogo, haja kubwa, vinyama vya ini na sampuli
za vyakula zilipelekwa katika maabara za mkemia mkuu wa serikali,
maabara ya mamlaka ya chakula na dawa ‘TFDA’
>>>’Hadi
sasa sampuli za nafaka pekee, zilizofanyiwa uchunguzi katika maabara ya
TFDA ndio zilizoonyesha kuwepo kwa uchafuzi wa sumukavu ‘Aflatoxin’
katika sampuli za nafaka hizo’:- Waziri Mwalimu
Waziri
ameongeza pia kuna uwezekano mkubwa kwamba ugonjwa huo umesababishwa na
ulaji wa chakula kilichokuwa na sumukuvu na kuleta madhara.
Post a Comment