LIWALE SUPER CUP
2016,
Ligi ya Liwale super cup leo June 22 limeanza kutimua vumbi katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi,katika ligi hii kuna timu 12 zilizothibitisha kushiriki.
leo kulikuwa na mchezo wa ufunguzi kati ya timu ya Bodaboda fc Vs Sido fc
mchezo uliochezwa katika uwanja wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Katika kipindi cha kwanza timu ya Sido fc iliongoza kupata goli namo dakika ya 42 goli lilofungwa na Yunusu Mbonde goli hilo lilidumu mpaka mapunziko ya dakika 45
Timu ya Sido fc ilitumia vema basi zilizopigwa na iliweza kuongeza goli
Katika kipindi cha pili katika dakika ya 69 goli lililofungaa na Haikosi Mpwate.
Dakika ya 72 Abdulahi Badi mchezaji wa Bodaboda fc alipewa kadi nyekundi kwa kuonesha utovu wa nidhamu na kuigharimu timu ya Bodaboda fc kucheza wakiwa pungufu kwa mchezaji mmoja.
Dakika 90 za mchezo zinakamilika matokeo yalikuwa yanasomeka
Bodaboda fc 0-2 Sido fc.
Kocha wa timu ya Sido fc Mohamedi Hema alisema ameanza kutoa dozi kama kawaida nae kocha wa Bodaboda fc Waziri Likwawatu alisema mcheza wa leo kwa upande wao walicheza vizuri lakini walizidiwa ujanja wa kimchezo lakini anamatumaini ya kuweza kushinda mchezo ujao kwakuwa kikosi chake kina wachezaji wazuri.
Kesho ligi itaendelea kwa mchezo mmoja kati ya Kigamboni fc dhidi ya Likombora fc mchezo unaotarajia kuwa mkali zaidi mchezo huo utapigwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale majira ya saa 10 jioni.
Post a Comment