Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh.Jordan Rugimbana amesema kuwa kwa mwezi wa Tatu na wa nne wamebaini kuwa shillingi Bilioni Moja na millioni mia nane zimetumika kuwalipa wafanyakazi hewa jambo ambalo ni hasara kubwa sana kwa serikali.
Rugimbana ameyaeleza leo mjini Dodoma leo wakati akiongea na wazee wa Baraza la wazee Dodoma wakati wa mkutano wake wa kwanza na wazee wa Dodoma mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa huo.
Rugimbana amesema kuwa pamoja na kuhakikisha kuwa anafuatilia mambo mbalimbali ya kimaendeleo Mkoani Dodoma ni dhamira yake kuhakikisha kuwa wakazi na wazee wa Dodoma wanaboreshewa maisha ikiwa ni pamoja na zile za afya.
Aidha Mh. Rugimbana amesema kuwa kuna watu wanahujumu serikali kwa kuficha Sukari ambayo ipo na serikali imekwisha agiza hivyo amewataka wazee washirikiane kulaani vikali wanaoficha sukari hasa katika kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa Ramadhan na hatosita kumwondoa mfanyabiashara kama huyo Mkoani Dodoma.
Post a Comment