Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni amesema kwamba ujenzi wa
nyumba za polisi katika jiji la Mwanza ambazo zina uwezo wa kukaa
familia 24 zitakamilishwa katika mwaka wa fesha 2016 & 2017.
Masauni ameyasema hayo alipokuwa
akijibu swali la Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula aliyetaka kujua
ahadi ya serikali ya kujenga nyumba za polisi jiji la Mwanza ndani ya
wiki 36 ambapo nyumba hizo hazikukamilika na kuleta usumbufu mkubwa wa
makazi kwa askari polisi.‘’Tumetenga
fedha kwa ajili ya kukamilisha mradi huu na serikali itakamilisha na
miradi mingine ya nyumba za polisi zenye uwezo wa kubeba familia 12’’
Amesema Naibu Waziri Masauni.
Aidha Naibu Waziri amesema kukamilishwa
kwa nyumb hizo kutaenda sambamba na ujenzi wa nyumba za polisi katika
mikoa 17 kama serikali ilivyoahidi ili kusaidia kutatua kero ya muda
mrefu ya makazi ya polisi.
Post a Comment