0

EURO2016: FULL RATIBA YA 16 BORA

Mechi katika hatua ya makundi zimeanza kumalizika jana, sasa inafuata hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro 2016. Ni baada ya mechi kali na za kusisimua zilizoshuhudia Ureno na Ireland zikipenya dakika za mwisho .

Kuna mechi kadhaa ambazo zinaturudisha kwenye historia ya mashindano haya na zinatarajia kuwa na presha kubwa kuanzia kwa wachezaji, mabenchi ya ufundi na hata mashabiki pia.

Italy vs Spain inatarajiwa kuwa mechi kali mchezo ambao unazirejesha timu hizo kwenye kumbukumbu ya mchezo wa fainali ya Euro 2012 ambao Spain walishinda kwa bao 4-0.

Spain pia iliifunga Italy kwenye michuano ya Euro 2008, kwa hiyo Italy vichwani mwao watakuwa na kibarua cha kulipa kisasi watakapokutana siku ya Jumatatu.

Ufaransa vs Ireland ni game nyingine ianayotazamwa kwa uzito wa aina yake licha ya Ireland kuonekana kama vibonde mbele ya Ufaransa. Goli la mkono la Thierry Henry bado linawakumbusha machungu Ireland pale waliposhindwa kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia.

HII NDIO RATIBA KAMILI YA EURO 2016

Switzerland vs Poland (Jumamosi)

Wales vs Northern Ireland (Jumamosi)

Croatia vs Portugal (Jumamosi)

France vs Republic of Ireland (Jumapili)

Germany vs Slovakia (Jumapili)

Hungary vs Belgium (Jumapili)

Italy vs Spain (Jumatatu)

England vs Iceland (Jumatatu)

Post a Comment

 
Top