0
            
Vyanzo vya polisi na hospitali nchini nchini Israeli vimesema raia wawili wa Palestina wamepiga risasi katika mji wa Tel Aviv, na kuuwa watu wanne.

Kitengo cha huduma ya dharura kwa wagonjwa kimesema watu wengine kumi na tatu wamejeruhiwa baada ya tukio hilo lililotokea katika duka kubwa katikati ya mji, kando na wizara ya ulinzi ya Israel.

Washukiwa wa shambulizi hilo wote wametiwa mbaroni, huku mmoja akiwa amejeruhiwa kutokana na risasi.

Mwandishi wa BBC ambaye yuko mjini humo amesema mashambulizi ya aina hiyo hayatokei mara kwa mara mjini Tel Aviv.

Post a Comment

 
Top