Dar es Salaam. Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe,
Profesa Honest Ngowi amesema ongezeko la kodi ya VAT kwa miamala ya simu
itawaumiza wananchi wengi wanaotegemea huduma hiyo kama njia rahisi ya
kutuma na kupokea fedha.
“Ni wazi kwamba kodi hiyo inamuumiza mlaji. Awali waliweka kwa mpokeaji tu ndiyo anakatwa hela ya kutolea, lakini kwa sasa anayetuma pia atakatwa,” alisema Profesa Ngowi.
Profesa Ngowi alikwenda mbali zaidi akisema hata ongezeko la kodi kwa sekta ya utalii, linaweza kuathiri uchumi kwa sababu watalii wengi watakwepa kuingia nchini na kwenda nchi za jirani ambako kuna unafuu wa kodi.
Ofisa Habari wa Benki ya NMB, Vicent Mnyanyika alisema wanafanya uchambuzi wa bajeti ili kujua kiwango cha faida na athari itakayopatikana kwa uamuzi huo.

Post a Comment