Mwanariadha mlemavu
wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amefikishwa mahakamani bila ya miguu
yake ya bandia, wakati wa kusikizwa na kuamuliwa kwa kesi ya mauwaji
yanayomkabili.
Mwanariadha huyo alisimama kizimbani kwa mikongojo,
akiinamisha kichwa chake, huku wakili wake Barry Roux, akirejelea
kilichotukia usiku wa mauwaji ya mpenziwe Reeva Steenkamp, miaka mitatu
iliyopita.Alisema kuwa Bwana Pistorius, alipoteza kila kitu na hatoweza kurejelea taaluma yake tena ya kukimbia.
Binamu wa Bi Steenkamp, Kim Martin, aliiambia mahakama hiyo kuwa mwanariadha huyo amekataa kuelezea namna mauwaji hayo yalivyotekelezwa.
Post a Comment