Maofisa wa serikali nchini Libya
wanaarifu kwamba watu ishirini na watano wameuawa na maelfu wengine
wakijeruhiwa katika mlipuko uliotokea kwenye duka la kuhifadhia risasi
upande wa magharibi ya mji wa Garaboulli.
Duka hilo la kuhifadhia
silaha linaarifiwa kuwa lilikuwa likitumiwa na jeshi la nchi hiyo
lililoko katika mji wa Misrata, mji ulioko karibu na pwani.Inaarifiwa chanzo cha vifo vya watu hao ishirini na watano ni ugomvi uliozusha mapigano baina yao na wakaazi wa mji wa Garaboulli.
Mlipuko huo ulitukia mara tu baada ya wenyeji wa mji huo walipoingia katika duka hilo lililotelekezwa. Na mpaka sasa bado chanzo cha mlipuko huo hakijafahamika.
Mzalishaji vipindi wa BBC aliyekuwa karibu na eneo la tukio ameeleza kwamba barabra ya pwani mwa Garaboulli imefungwa na kwamba anasikia sauti za milio ya risasi kwa mbaali.
mchanganyiko wa raia wenye silaha na wanamgambo kutoka mji wa pwani wanaendesha upekuzi kwenye vituo vya ukaguzi kando kando ya barabara ya pwani, na magari yanayojaribu kupita eneo hilo yanafanyiwa upekuzi mkali ingawa haijajulikana wanapekuliwa kwa suala gani.
Katika sakata hilo inasemekana mmiliki na muuzaji wa duka hilo alipigwa risasi na kufariki dunia na baadaye kuliripotiwa mapigano ya kulipiza kisasi kati ya wanamgambo na wakaazi wa eneo hilo .
Duka hilo lililokuwa chanzo cha tatizo lilichomwa moto baadaye na nyumba ya familia ya mmiliki wa duka hilo iliyokuwa jirani,na baada ya tukio hilo wakazi wengine wenye silaha walipinga mashambulizi hayo na uwepo wa jumla wa wanamgambo kwamba na wakati huo huo duka la jirani lenye kuuza silaha pia lilikuwa na malori yenye mzigo wa biashara hasa vilipuzi liliripuka.
Post a Comment