Nyota wa soka wa
timu ya Argentina na Barcelona Lionnel Messi anatarajiwa kutoa ushahidi
katika mahakama ya Uhispania kuhusu mashtaka ya kukwepa kulipa ushuru.
Messi
na Babake Jorge ambaye anasimamia maswala yake ya fedha wanatuhumiwa
kuilaghai Uhispania zaidi ya yuro milioni 4 kati ya mwaka 2007 na 2009.Mamlaka inadai kuwa wawili hao walitumia kampuni zao zilizopo Belize na Uruguay kuficha mapato yao yanayotokana na haki za picha zao.
Mamlaka ya ushuru nchini Uhispana inataka mchezaji huyo kupigwa faini kubwa pamoja na kufungwa jela.
Wawili hao wamekana kutekeleza uhalifu huo.
Post a Comment