0

Matokeo ya awali ya kura ya maoni iliyopigwa hapo jana kuhusu Uingereza kujitoa au kubakia ndani ya Umoja wa Ulaya yameanza kutolewa.
Hadi sasa ni majimbo machache ndio yametangaza matokeo yao na inaonyesha mchuano ni mkali kati ya wanaotaka kubakia na wale wanaotaka Uingereza kujiondoa ndani ya Umoja huo wa Ulaya.
Kwa mujibu wa ripoti waliojitokeza kupiga kura hiyo ya maoni inaonyesha kuwa wengi.
Sarafu ya Euro imepanda katika masoko ya fedha huku Paundi ya Uingereza ikiendelea kuporomoka ikiwa ni ishara kuwa wafanyabiashara wanatarajia Uingereza kubakia ndani ya Umoja wa Ulaya.

Post a Comment

 
Top