Muthama akielekea katika kituo cha polisi kutoa taarifa
Wabunge sita nchini Kenya wanatarajiwa kuwasilishwa mahakamani kufuatia madai ya kutoa matamshi ya chuki.
Siku
ya Jumapili mbunge mmoja anayegemea upande wa serikali alidaiwa kutaka
kuuawa kwa aliyekuwa waziri mkuu na kiongozi wa upinzani nchini humo
Raila Odinga.
Wabunge hao ni Moses Kuria, Kimani Ngunjiri na
Ferdinand Waititu kutoka kwa upande wa serikali na Junet Mohammed Aisha
Jumwa,Johnson Muthama na Timothy Bosire upande wa upinzani.
Bw Kuria anadaiwa kuitisha kuuawa kwa Raila kupitia lugha ya kikikuyu.Hathivyo amekana kutoa matamshi hayo.
Wabunge
wa Upinzani walifanya mkutano na wanahabari siku ya Jumatatu na kutoa
wito kwa wafuasi wa chama hicho kulinda uongozi wa chama hicho kwa kuwa
serikali imeshindwa kufanya hivyo.
Polisi wamesema kuwa tamko
hilo ni la chuki.Wanne hao wanatoa ushahidi katika kituo kimoja cha
polisi katika mji mkuu Nairobi.Wabunge watatu wa Jubilee walitoa
matamshi hayo usiku wa kumia Jumanne.
Mkuu wa idara ya jinai Ndegwa Muhoro amewaambia waandishi kwamba polisi watamkamata mtu yeyote anayeeneza matamshi ya chuki.
Post a Comment