Mamlaka ya Misri
inasema mabaki ya ndege ya EgyptAir ambayo ilianguka katika bahari ya
Mediteranian mwezi uliopita ikiwa imebeba abiria sitini na sita yameweza
kubainika yalipo.
Katika maelezo yaliyotolewa na kamati husika ya
uchunguzi wa ajali hiyo wanasema ,meli inayotafuta mabaki ya ndege ya
EgyptAir imeweza kubaini maeneo kadhaa ambayo mabaki ya ndege ya A320
yapo na kutoa picha ya kwanza ya masalio hayo.
Kwa sasa kikosi
hicho cha wakaguzi walioko melini watachora ramani wakionesha vielelezo
vya mabaki ya ndege yalivyoeneo. Ndege hiyo iliyopotea baada ya
kutoonekana kwenye rada wakati ikiwa inatokea Paris kuelekea Cairo. Huku
ikiwa inadhaniwa kuwa lilishambuliwa na bomu.Lakini hakuna kikosi
chochote cha kigaidi kilichodai kuhusika na kuangusha ndege hiyo.
Post a Comment