Omar el bashir
Kitengo cha usalama
nchini Sudan kimewaachiliwa huru wanafunzi sita wanaofanya uanaharakati
waliokuwa wakizuiliwa bila mashtaka tangu msururu wa maandamano katika
mji mkuu mnamo mwezi Mei, wakili wao amesema.
Maandamano hayo
ghasia isababisha mamia ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Khartoum
kukabiliana na vikosi vya usalama huku wakiandamana dhidi ya sera za
serikali na kutaka kuwachiliwa kwa waandamanaji walioandamana.
Wanafunzi
sita ambao ni wanaharakati wa kijamii wameachiliwa huru lakini wengine
wanane wangali wanazuiliwa na idara ya ujasusi nchini Sudan NISS.
Vyanzo
vya kibalozi ambavyo viko karibu na familia ya wanafunzi hao
vimethibitisha kuwa wanafunzi hao wameachiliwa na vimesema kuwa wale
walioko kizuizini huenda wakafunguliwa mashtaka.
Wakili wa
wanafunzi hao amesema kuwa mazungumzo yanaendelea ili kujaribu
kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanarejelea masomu yao katika chuo kikuu
baada ya kutimuliwa na wasimamizi kufuatia maandamano hayo.
Shirika la NISS lina mamlaka makubwa na katika miezi
ya hivi karibuni, limewasaka wanafunzi ambao wamekuwa wakifanya
maandamano na migomo katika vyuo vikuu. Aprili mwaka huu wanafunzi
wawili waliuawa wakati walipokuwa wakiandamana.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadam yameelezea wasi wasi kuhusiana na usalama wa wanafunzi hao ambao wako kizuizini.
Shirika
la kimataifa la haki za kibinadam International Federation of Human
Rights (FIDH) limesema kuwa limenakili visa kadhaa vya wanafunzi hao
kudhulumiwa pamoja na wafungwa wengine.
Post a Comment