0

Mkazi wa kijiji cha Negero, Ole Mollel (61) akiwa kwenye zahanati ya kijiji hicho baada ya kumsindikiza mkewe mjamzito, Nai Mollel (18) kwa ajili ya vipimo siku ya kliniki. Picha na Tumaini Msowoya

Kilindi. Idadi ya wanaume wanaohudhulia kliniki kwa ajili ya kuwasindikiza wake zao wakiwa wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano imeongezeka hadi kufikia asilimia 99, wilayani Kilindi Mkoa wa Tanga.

Akifunga mradi wa Afya ya Mama na Mtoto uliokuwa ukitekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania (WVT), wilayani humo, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa amesema idadi hiyo ni kubwa ikilinganishwa na ya awali.

Amesema wanaume walikuwa wakiamini masuala hayo ni ya wanawake.

Liwowa amesema hali hiyo itasaidia kutekeleza mkakati huo wa kupunguza ongezeko la vifo vya mama na mtoto.

Amesema wanaume wanaposhiriki moja kwa moja kwenye masuala ya uzazi na malezi ya watoto, wanasaidia kujenga jamii imara.

Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kwediboma wilayani humo, Nurdin Mgaza amesema imekuwa kawaida siku hizi kuona kila mwanamke anapokwenda zahanati anaongozana na mumewe.

Meneja wa mradi wa mama na mtoto wa World Vision, Daudi Gambo alimesema kazi waliyokuwa wakiifanya ni kuhakikisha wanaume wanashiriki kwenye malezi ya familia badala ya kumuachia mwanamke. 

Hata hivyo aliiomba Serikali kuendelea kuwaelimisha wanaume umuhimu wa kujali familia zao kwa kuhusika kwenye malezi na masuala ya uzazi, jambo litakalopunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kiwango kikubwa.MWANANCHI

Post a Comment

 
Top