0


Dar es Salaam. Licha ya kukabiliwa na uhaba wa damu, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), inakumbana na changamoto ya vifaa vya kuhifadhia damu inayokusanywa ikiwamo jokofu la kibaolojia.

 Kutokana na hali hiyo hakuna uhifadhi mathubuti wa damu.

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Makwaia Makani amesema hayo wakati Balozi wa China hapa nchini, LU Youqing akichangia damu hospitalini hapo ikiwa ni mchango wake katika kuadhimisha Siku ya Uchangiaji Damu duniani ambayo kwa hapa nchini kitaifa ilifanyika mkoani Dodoma.

 Amesema Muhimbili inakusanya chupa za damu kati ya 60 hadi 100 kwa siku, lakini bado ina upungufu wa vifaa kadhaa vya ukusanyaji na vipimo vya kupimia.

Post a Comment

 
Top