0

Mapema mwezi Machi mwaka huu kumeripotiwa migomo na maandamo ya mfululizo nchini Ufaransa, licha ya jitihada za serikali ya nchini humo kujaribu kufanya jitahada za kuumaliza lakini vyama  vya wafanyakazi nchini Ufaransa vimetangaza kuongeza kasi ya kundelea kuanzisha migomo nchini humo.

Mbali ya shughuli za uzalishaji kupungua sasa mgomo huo  umesababisha kuzagaa kwa taka nchini Ufaransa.

Mgomo uliosababishwa na sheria mpya ya wafanyakazi nchini Ufaransa  umesababisha taka kuzagaa na barabara kusalia chafu.

Wafanyakazi katika kituo kikubwa cha urejeshaji taka Ivry-Paris 13 Ufaransa waliitikia mgomo na kupelekea taka kuzagaa katika mitaa tangu Jumanne wiki iliopita.

Kila siku takriban tani 2,000 za taka husafirishwa kwa kutumia malori 200 ambapo kwa sasa kutokana na mgomo huo taka zimesalia barabarani na kusababisha uchafu.

Mmoja miongoni wa wafanyakazi katika kituo hicho amefahamisha kuwa alijiunga na wenzake kupinga sheria mpya inayowakandamiza wafanyakazi na kusema kuwa wataendelea kuandamana hadi sheria hiyo pale itakapoondolewa.

Post a Comment

 
Top