Mtu mmoja nchini
Chicago alipigwa risasi akiwa katika video ya moja kwa moja
inayojulikana kama Live_stream katika mtandao wa Facebook ,polisi
wamesema.
Antonio Perkins mwenye umri wa miaka 28 alipigwa risasi katika kichwa na shingo magharibi mwa mji huo.
Kanda hiyo ya video bado iko katika facebook na imeangaliwa mara 700,000.
Ni
mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu mjini Chicago
ambapo mauaji yamefanyika moja kwa moja katika mtandao wa facebook.
Mnamo mwezi Machi mtu asiyejulikana alipigwa risasi mara 16 wakati akipeperusha matangazo hewani.
Hakuna mtu aliyekamatwa kufika sasa.Programu ya live-streaming ya facebook inawaruhusu watu kutangaza moja kwa moja mtandaoni .
Post a Comment