Kwa
Munaasabah wa mwezi mtukufu wa Ramadhwaan, Alhidaaya
imewawekea tayari mafundisho mbalimbali yenye manufaa
katika kuongeza elimu na kuimarisha 'ibaadah zenu ili
muweze kuchuma mema mengi na muweze kufikia kuipata taqwaa
ambayo ndio lengo kuu la Swawm.
Fadhila Na Faida Za Qiyaamul-Layl
Mtume (Swalla
Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:
((من قام
رمضان
إيماناً
واحتساباً
غفر له ما
تقدم من
ذنبه)) متفق
عليه
((Atakayesimama (Kuswali)
Ramadhaan kwa imaani na kutaraji malipo, ataghufuriwa
madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy na
Muslim]
Al-Haafidh Ibn Rajab
(Rahimahu Allaah) amesema:
"Tambua kuwa Muumini
anajumuisha katika mwezi wa Ramadhaan jihaad mbili kwa
ajili ya nafsi yake; jihaad ya mchana ya kufunga, na jihaad
ya usiku kwa kusimama (kuswali), atakayejumuisha jihaad
hizi mbili atapata ujira wake bila ya
hesabu".
Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu
Allaah) amesema:
"Haimpasi Muislamu
kuepukana na Swalah ya Tarawiyh katika Ramadhaan ili apate
thawabu na ujira wake, na wala asiondoke mpaka Imaam amalize
Swalah ya Witr ili apate ujira kamili wa
Qiyaamul-Layl".
|
|||
Hadiyth Al-Qudsiy - Hadiyth Ya 18 - Swawm Ni Yangu Na Ni Mimi Ndiye Ninayelipa
عَنْ
أَبِي
هُرَيْرَةَ
عَنْ
النَّبِيِّ
صَلَّى
اللَّهُ
عَلَيْهِ
وَسَلَّمَ
قَال:
((يَقُولُ
اللَّهُ
عَزَّ
وَجَلَّ:
الصَّوْمُ
لِي
وَأَنَا
أَجْزِي
بِهِ،
يَدَعُ
شَهْوَتَهُ
وَأَكْلَهُ
وَشُرْبَهُ
مِنْ
أَجْلِي،
وَالصَّوْمُ
جُنَّةٌ
وَلِلصَّائِمِ
فَرْحَتَانِ،
فَرْحَةٌ
حِينَ
يُفْطِرُ
وَفَرْحَةٌ
حِينَ
يَلْقَى
رَبَّهُ،
وَلَخُلُوفُ
فَمِ
الصَّائِمِ
أَطْيَبُ
عِنْدَ
اللَّهِ
مِنْ
رِيحِ
الْمِسْكِ)) البخاري
و مسلم و
مالك
والترمذي
والنسائي
وابن
ماجه
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu
‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye alisema: ((Allaah
Aliyetukuka na Jalali Anasema: Swawm ni Yangu na ni Mimi
ndiye ninayelipa. (Mtu) huacha matamanio yake, chakula
chake, kinywaji chake kwa ajili Yangu. Swawm ni ngao, na
yule anayefunga ana furaha mbili; Furaha anapofuturu na
furaha anapokutana na Mola wake. Mbadiliko wa harufu ya
pumzi zake (kutoka mdomoni) ni bora kwa Allaah kuliko harufu
ya misk)) [Al-Bukhaariy, Muslim,
Maalik, At-Tirmdihiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]
|
|||
Kila Mtu Ataingia Peponi Isipokuwa Anayekataa
Allaah (Subhaanahu wa
Ta’ala) Amewaumba majini na watu kwa lengo la
kumuabudu Yeye Pekee. Wala Hakuwaleta duniani kuja kufanya
masikhara na kuumaliza muda wao bila ya mambo ya
msingi.
|
|||
|
|||
QUR-AAN Mahmuwd Al-Huswariy (Warsh) MAWAIDHA Abuu Haatim 'Abdullaah Abuu Usaamah Farah |
|||
|
|||
|
Post a Comment