Romelu Lukaku
alifunga mabao mawili huku timu ya taifa la Ubelgiji ikipata ushindi
wake wa kwanza katika michuano ya Euro2016 na kuharibu fursa ya timu ya
Jamhuri ya Ireland kufika robo fainali.
Baada ya kukamilika kwa
kipindi cha kwanza ambapo hakuna timu ilioona lango la mwengine,Lukaku
aliifungia Ubelgiji bao la kwanza baada ya kupata pasi muruwa.
Baadaye Axel Witsel alifunga bao la pili kupitia
kichwa katika dakika ya 61,kabla ya Lukaku kufunga bao la tatu baada ya
kushambulia ngome ya Ireland.
Timu ya Jamhuri ya Ireland ilishindwa kufanya mashambulio katika ngome ya Ubelgiji.
Post a Comment