0
                                

Mwaandishi wetu
Tanesco mkoani Lindi imetakiwa kuboresha  utendaji kazi wake ili kuondoa hadhi na hasara kwa wananchi kutokana na kukatika katika kwa umeme.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa  Lindi Godfrey Zambi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa fisi-Lindi.
Zambi amesema kitendo cha kukatika katika kwa umeme mara kwa mara bila taarifa kunachingia uharibifu na kuungua kwa mali  vifaa vya wananchi.
Amesema  kipindi alichopo mkoani Lindi hajawahi kufaidi na kuona umeme umetulia bila itilafu na kusikitishwa  na tukio la  siku moja alipoona umeme umekatika  zaidi ya  mara 12. 
Zambi  amelitoa agizo hilo baada ya wananchi wa Manispaa ya Lindi  kulalamikia tanesco  kukatika kwa umeme mara kwa mara na  kutotoa taarifa ya tatizo hilo  wannanchi linapotokea.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa  Tanesco mkoa wa Lindi Naomi Mwaipula amesema kukatika kwa umeme kunatokana na kuwepo kwa miundo mbinu chakafu hivyo shirika  lianza kufanya  marekebisho ya kuondoa miundombinu chakavu na kuweka mipya na zoezi litakamilika mapema ya desemba 2016.

Post a Comment

 
Top