Timu ya taifa ya Argentina bado inaongoza orodha ya kila mwezi ya FIFA ya timu bora duniani ambayo imetolewa Ijumaa.
Kwenye
orodha hiyo timu ya taifa ya Ubelgiji iko kwenye nafasi ya pili
ikifwatiwa na Chile.Ujerumani ni ya 5,ikifwatiwa na Uhispania na Brazil
inachukua nafasi ya saba.Timu ya bara la Afrika inayochukua nafasi nzuri kwenye orodha hiyo ya FIFA ni Algeria iliopo katika nafasi ya 33 ikifwatiwa na Ivory Coast katika nafasi ya 34.
Kwa nchi za Afrika mashariki Uganda 72;Rwanda 87 kenya 116 Burundi 122 na Tanzania inachukua nafasi ya 129 kwenye orodha hiyo ya FIFA.
Post a Comment