
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA), Irene Isaka, akimpatia maelezo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. John Magufuli wakati alipotembelea banda la mamlaka hiyo,
katika maonesho ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (May
Day), viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma jana.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, akimsalimia
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano cha Mamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, wakati
alipotembelea banda la mamlaka hiyo, katika maonesho ya maadhimisho ya
Siku ya Wafanyakazi Duniani (May Day), viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma
jana. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, akiwasalimia
baadhi ya Maofisa wa Mamlaka hiyo, alipotembelea banda la mamlaka hiyo,
katika maonesho ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (May
Day), viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma jana.
Post a Comment