MNAMO
TAREHE 22.05.2015 MAJIRA YA SAA 20:00HRS KATIKA MTAA WA BULALE KATA YA
BUHONGWA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MWENYEKITI WA MTAA
WA BUBALE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ALPHONCE MUSSA NYINZI MIAKA 48,
MSUKUMA MFANYABIASHARA NA MKAZI WA BULALE ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI
KIFUANI NA KUTOKEA CHINI YA KWAPA UPANDE WA KULIA NA WATU WAWILI WASIO
FAHAMIKA. RISASI HIYO PIA ILIMJERUHI NEEMA MARANGULA MIAKA 23 MKAZI WA
BULALE KATIKA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA.
INAELEZWA
KWAMBA SIKU HIYO JIONI ALIKUA AMETOKA KWENYE KIKAO ALICHOFANYA NA
WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WA MTAA WA BULALE, KATIKA MUDA WA
SAA 20:00HRS USIKU AKIELEKEA NYUMBANI AKIONGOZANA NA WAJUMBE WAWILI
ALIKUTANA NA NEEMA MARANGULA AKIWA NA MUME WAKE AMBAO WALIKUA
WANAWAFUATA MAREHEMU NA BALOZI KWA AJILI YA KUZUNGUMZIA MZOZO WA NDANI
YA NDOA YAO KWA HIYO WALIKUA WANAHITAJI KUSULUHISHWA, MAREHEMU NA
WAJUMBE WAKE WAWILI WAKIWA PAMOJA NA BI NEEMA PAMOJA NA MUMEWE WAKIWA
WANAJADILI TATIZO HILO HAPO BARABARANI MARA GHAFLA WAKATOKEA WATU WAWILI
AMBAO WALIKUA WAKIPITA BARABARANI NA KUWAAMBIA MKO CHINI YA ULINZI NA
MMOJA WAO AKATOA BUNDUKI NA KUMPIGA RISASI MAREHEMU AMBAYE ALIANGUKA
CHINI HUKU WENZAKE WAKIKIMBIA KUJIOKOA KUTOKA ENEO HILO LAKINI PIA WALE
WAHALIFU WAKAKIMBIA NA KUTOKOMEA GIZANI VICHAKANI.
NDIPO
WANANCHI WA ENEO HILO WALIJITOKEZA KWA MSAADA WA KUMSAIDIA MAREHEMU,
WALIMCHUKUA MAREHEMU KUMKIMBIZA HOSPITALI KWA MATIBABU LAKINI ALIFARIKI
DUNIA WAKIWA NJIANI. MAJERUHI BI NEEMA MARANGULA AMELAZWA HOSPITALI YA
MKOA WA MWANZA SEKOU TOURE KWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.
MWILI WA MAREHEMU UPO HOSPITALI MKOA WA MWANZA SEKOU TOURE KWA AJILI YA
UCHUNGUZI WA DAKTARI. CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA,
UCHUNGUZI TUKIO HILO BADO UNAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA JESHI LA
POLISI AHMED MSANGI ANAWAOMBA WANANCHI WENYE TAARIFA ZOZOTE KUHUSIANA
NA TUKIO HILO ZITAKAZO SAIDIA KUFANIKISHA KUKAMATA WAHUSIKA WAZITOE
POLISI LAKINI PIA KUTOA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI WAO NA KUHAKIKISHA
WANATENGENEZA MAKAZI SALAMA HUKO WANAPOISHI NA MAENEO YA SHUGHULI ZAO.
MSAKO MKALI UNAFANYIKA NA KUHAKIKISHA WAHUSIKA WA TUKIO HILO
WANAKAMATWA.
IMETOLEWA NA:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
BREAKING NEWS:VAN GAAL ATIMULIWA MAN UNITED
Daily
Mail limeripoti kwamba klabu ya Manchester United imemfuta kazi rasmi
aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Louis van Gaal ikiwa ni siku mbili tu
tangu Mdachi huyo awape ubingwa wa kombe la FA baada ya kuwafunga
Crystal Palace 2-1.
Sababu
kubwa za kufutwa kwake kazi ni kutofikia malengo ya klabu hiyo kwenye
msimu huu wa ligi uliomalizika. Nafasi ya Van Gaal itazibwa na aliyekuwa
kocha wa Chelsea Jose Mourinho.
Van Gaal amefukuzwa pamoja na jopo lake lote akiwemo msaidizi wake Albert Stuivenberg na kocha wa makipa Frans Hoek.
BREAKING NEWS:VAN GAAL ATIMULIWA MAN UNITED
Daily
Mail limeripoti kwamba klabu ya Manchester United imemfuta kazi rasmi
aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Louis van Gaal ikiwa ni siku mbili tu
tangu Mdachi huyo awape ubingwa wa kombe la FA baada ya kuwafunga
Crystal Palace 2-1.
Sababu
kubwa za kufutwa kwake kazi ni kutofikia malengo ya klabu hiyo kwenye
msimu huu wa ligi uliomalizika. Nafasi ya Van Gaal itazibwa na aliyekuwa
kocha wa Chelsea Jose Mourinho.
Van Gaal amefukuzwa pamoja na jopo lake lote akiwemo msaidizi wake Albert Stuivenberg na kocha wa makipa Frans Hoek.
Post a Comment