Mama
mmoja amedai kupigwa na muuguzi wakati akijifungua katika hospitali ya
Rufaa Meta ya jijini Mbeya na baada ya kujifungua muuguzi huyo
akamchukua mwanae mchanga na kumtupia kifuani jambo ambalo amesema
lilihatarisha uhai wa mwanae.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amefanya ziara ya kustukiza
katika hospitali ya Rufaa ya wazazi Meta ya jijini Mbeya na kushuhudia
msongamano mkubwa wa akina mama wajawazito hospitalini hapo, na
alipofika katika chumba cha akina mama ambao wanasubiri watoto wao ambao
wamewekwa katika chumba maalum cha joto, ndipo akakutanana na
malalamiko ya mama Salome Waya ambaye amedai kupigwa na muuguzi wakati
akijifungua.
Kufuatia madai hayo, mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akalazimika
kupitia nyaraka za mama huyo ili kumtambua muuguzi aliyemfanyia ukatiri
huo na akafanikiwa kumbaini kuwa anaitwa Beatrice Sanga ndipo akatoa
agizo kwa mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya kanda ya nyanda za juu
kusini, Dk. Goodlove Mbwanji kufanya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi
ya muuguzi huyo ndani ya siku saba.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk. Goodlove Mbwaji amesema kuwa
katika mazingira hayo hawezi kujitetea na badala yake atazingatia
maelekezo ambayo amepewa na mkuu wa mkoa.
Post a Comment